Header Ads

Joketi apangua majigambo ya Wema Sepetu Instagram

 Mrembo msomi na mjasiliamali Joketi Mwegelo ametikisa mtandao wa kijamii wa Instagram kwa kupost picha zake ambazo yeye anaamini ndio Jokate Original ukiacha wa kwenye magazeti. Mwanadada huyo amepost picha hizo na kuambatanisha na ujumbe chini yake ukionesha majigambo ya uzuri wake. Picha hizi zimekua gumzo na wadau mbalimbali wameweza kutafsiri kama majibu kwa mwanadada Wema Sepetu.


Katika mtandao wa instagram alipoweka picha hizo, moja ameandika The Original. The OG#Kidoti, kisha nyingine, African Barbie. African Queen. Tazama picha hapa chini.

Kumekuwa na majigambo ya ushindani wa picha kati ya mastaa mbalimbali kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo hivi karibuni tumemuona mwanadada Wema Sepetu akiandika ujumbe wa kuringia shepu yake na uzuri wake, kupitia ukurasa wa Instagram aliandika 
  • 'wemasepetuShepu ya mwendokasi... Ndo niliojaliwa nayo... Kama imeanzia kiunoni kwenda magotini ndo niliojaliwa nayo... Kama wewe hauna basi mshukuru Allah... Ndo nilivyoumbwa jamani... Sio mimi bali ni Maulana ndo alionibariki nayo... Hata ingekuwa kwanzia kichwa hadi Vidole vya miguuni ni sawa pia... Ndo niliojaliwa nayo.... Sometimes najiangalia kwenye kioo sijimalizi... Ndo majaliwa yangu... Ndo yangu basi... Imenizidia... Allah Subhanah wataallah ndo amenipa... Aaaah....!? Sio shepu ya kawaida... Niacheni na Shepu yangu jamani... Ndo nishaimiliki mie... Siwezi kuitoa...'


No comments:

Powered by Blogger.