MAGUFULI ADAMKIA MUHIMBILI
Magufuli adamkia Muhimbili
Rais
John Magufuli na Mkewe, Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali mtoto
Shukuru Kisonga aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jana.
Shukuru alikuwa akiishi kwa kula sukari, maziwa na mafuta ya kula. Hali
yake kwa sasa inaendelea kuimarika na kuanza kula vyakula vya kawaida.
Katikati ni Mama yake Shukuru, Mwanahabibi Mohamed Mtei.
Aidha, ameelezwa kuwa hospitali hiyo imepiga hatua kubwa ya kujenga uwezo wa kutibu magonjwa ambayo wagonjwa walilazimika kwenda kutibiwa nje ya nchi na hivyo kuokoa fedha nyingi za serikali; na kwamba kuanzia Julai mwaka huu, itaanza kupandikiza figo.
Kwa muijibu wa Ikulu, Rais Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli waliwatembelea wagonjwa hao saa moja asubuhi wakitokea katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam ambako walihudhuria ibada ya Jumapili.
Miongoni mwa wagonjwa waliojuliwa hali na Rais Magufuli na mkewe ni Mzee Francis Kanyasu (Ngosha), mzee anayeaminika kubuni Nembo ya Taifa ambaye amelazwa katika chumba namba 310 na mtoto Shukuru Kisonga aliyelazwa katika chumba namba 312 ambaye hivi karibuni aliripotiwa kuugua ugonjwa usiofahamika uliosababisha aishi kwa kunywa mafuta ya kula, sukari na maziwa.
Pamoja na kuwapa pole wagonjwa waliolazwa katika wodi ya Mwaisela na kuwashukuru madaktari na wauguzi, Rais Magufuli alisema serikali itaendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili hospitali hiyo na changamoto zinazowakabili madaktari na wauguzi.
“Jamani, madaktari tunawashukuru sana, mnafanya kazi nzuri, madaktari wote nchini pokeeni pongezi zangu, sisi serikali tutaendelea kuzikabili changamoto hizo na siku moja zitakwisha, kikubwa ni kumtanguliza Mungu mnapofanya kazi ya kuokoa maisha ya watu kwa juhudi kubwa, mnafanya kazi ya Mungu,” alisema Rais Magufuli.
No comments:
Post a Comment